Leo, tarehe 28 Agosti 2025, MUCE ilipata heshima ya kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Kheri James, aliyefika Chuoni kuangalia maendeleo ya miradi ya ujenzi wa miundombinu mipya inayotekelezwa na Chuo. Katika ziara hiyo, kabla ya kutembelea miradi ya ujenzi, Mkuu wa Mkoa alipewa taarifa ya safari ya Chuo, mafanikio yake, na mchango wake katika kukuza elimu ya juu nchini.
TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA YA WANATAALUMA
Tarehe: 28 Agosti 2025
Naibu Rasi wa Mipango, Fedha, na Utawala wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)
anawatangazia waombaji kazi walioufanya usaili tarehe 27 Julai 2025 kuwa matokeo ya
waliofaulu yamechapishwa. Waliofaulu wanapaswa kukamilisha taratibu za ajira kati ya
tarehe 28 Agosti hadi 11 Septemba 2025 kwa kufika MUCE wakiwa na nyaraka zilizoainishwa
katika tangazo hili ili zihakikiwe kabla ya kupewa barua za ajira. Wale ambao majina
yao hayapo kwenye tangazo wametaarifiwa kuwa hawakufaulu lakini wanakaribishwa kuomba
nafasi zitakazotangazwa baadaye.
Pakua tangazo la walioitwa hapa