MUCE Attends CEOs Workshop in Arusha
✨ Ushiriki wa MUCE katika Kikao Kazi Arusha ✨
Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kimehudhuria Kikao Kazi cha Watendaji Wakuu wa Taasisi na Wenyeviti wa Bodi kilichofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 23–26 Agosti 2025.
Kikao hicho kilifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Philip Isdory Mpango, na kufungwa na Naibu Waziri Mkuu, Mh. Doto Biteko.
Lengo kuu la kikao hiki lilikuwa ni kuwajengea washiriki uelewa na mbinu bora katika nyanja mbalimbali za kiutendaji, ikiwa ni pamoja na:
• Uboreshaji wa huduma ili kuongeza ufanisi katika taasisi za umma 💡
• Usimamizi bora wa fedha kwa kuzingatia uwajibikaji na uwazi 💰
• Miongozo ya kitaifa na kimataifa katika uendeshaji wa shughuli za taasisi 📑
• Kubadilishana uzoefu na mafunzo baina ya taasisi mbalimbali 🤝
Kwa upande wa MUCE, ushiriki huo uliwakilishwa na Rasi wa Chuo, Prof. Method S. Semiono, pamoja na Mwenyekiti wa Bodi, Prof. William A. L. Anangisye.
Kikao Kazi hiki kiliitishwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa ajili ya taasisi zote zilizo chini ya usimamizi wake, kikibaki kuwa jukwaa muhimu la kuimarisha uwajibikaji, usimamizi bora na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa wananchi.