Ujumbe karibishi kutoka kwa mkuu wa chuo
Ninafuraha kubwa kukukaribisha Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE),
chuo kishiriki cha Chuo kikuu cha Dar es Salaam kilichopo katika mji wa
kihistoria Iringa, Tanzania.
Hapa MUCE, tunajivunia kutoa digrii za awali na za uzamili zinazowapa wahitimu wetu si tu maarifa ya kitaaluma kinadharia,
bali pia ujuzi wa kivitendo unaohitajika ili kufanikiwa kwenye tasnia ya elimu inayobadilika kila uchao. Wana kitivo mahiri
na makini wanajitolea kudumisha viwango vya juu kabisa vya ufundishaji na utafiti, kuhakikisha kila mwanafunzi anapata
mazingira rafiki na jumuishi ya ujifunzaji.
Kama Mkuu wa Chuo, ninakualika ujionee utajiri wa fursa na rasilimali zinazopatikana MUCE. Ikiwa wewe ni mwanafunzi tarajali,
mzazi au taasisi mshirika, ninakuomba ujionee jinsi uwajibikaji wetu katika ujenzi wa elimu bora, uvumbuzi na huduma unavyoweza
kukusaidia kufikia matarajio yako.
Asante kwa kutembelea tovuti yetu. Tunatazamia kukukaribisha wewe binafsi na kukuongoza kuelekea kwenye mustakabali uliojengwa
na mafanikio ya kitaaluma na wenye matokeo yenye tija.
Prof. Method Samwel Semiono
Rasi, Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE)