Skip to main content

KUHUSU SISI

"Maarifa, Uadilifu na Ubora"

Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) ni taasisi inayotambulika kwa taaluma mbalimbali na yenye historia ndefu tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005 kama taasisi ya elimu ya juu. Taasisi hii ina vitivo vitatu na idara nane, zinazotoa huduma nyingi anuawai za kitaaluma na kitaalamu. Kwa kuwa elimu jumuishi ni kitovu cha dhamira yetu, chuo kina Kitengo cha Elimu ya Mahitaji Maalum, kinachotoa msaada na kuwawezesha kwa watu wenye mahitaji maalum.

MUCE ni jumuiya inayokua yenye wanafunzi 6,272 na wafanyakazi mahiri na makini 403. Miongoni mwa wafanyakazi hao, 213 ni wanataaluma. Kadiri inavyokua, MUCE inaendelea kuwa imara katika dhamira yake ya kutoa elimu bora, kukuza tafiti za uvumbuzi, na kuwa kichocheo cha mabadiliko chanya katika jamii.

Tunakualika/Tunakukaribisha ujionee mazingira yetu mazuri ya kitaaluma na uungane nasi katika safari yetu ya kuleta ubora wa kitaaluma na mageuzi ya kijamii

Katika Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa, tunaongozwa na dira bayana na maadili msingi yanaongoza dhamira yetu ya kujenga ubora na maendeleo endelevu.

Dira Yetu

Kuwa kituo cha kikanda cha ubora kinachochangia maendeleo endelevu kwa kutoa wahitimu wenye ujuzi na ari ya juu, matokeo ya tafiti za kiuvumbuzi na kutoa huduma bora kwa umma.

Dhamira Yetu

Kukuza ustawi wa jamii kupitia elimu bora, utafiti na huduma kwa umma.

Kauli Mbiu Yetu

Kukuza ubora, kujenga maendeleo endelevu.

Maadili Msingi

Ili kufikia dira na dhamira yake, Chuo kinakusudia kuzingatia maadili yafuatayo:
  • Ubora wa Kitaaluma: kufanya jitihada za kufikia viwango vya juu kabisa vya utendaji, ubunifu, kuonyesha uanataaluma, na kupata maarifa na ujuzi mpya.
  • Uhuru wa Kitaalama: Kudumisha uhuru wa kueleza mawazo ya kitaaluma bila kuwa katika hatari ya kuingiliwa au kudhuriwa na mamlaka.
  • Uzingatizi wa sifa: MUCE itafuata kanuni za kuzingatia sifa katika michakato yote ikiwa ni pamoja na ajira, uteuzi, kupandishwa cheo na manunuzi.
  • Uadilifu: Kuzingatia maadili, uaminifu, ukweli, bidii, kuwajibika katika majukumu ya kitaaluma na kuepuka mgongano wa maslahi.
  • Usawa: Kutengeneza mazingira yanayoleta ushirikiano katika kazi, ujumuishaji, ustawi wa kijinsia na unuai wa kitamaduni.
  • Ushirikiano: Kudumisha ubia wa kimkakati wa ndani na ushirikiano wa kimataifa katika tafiti na ubadilishanaji wa maarifa.
  • Kuwajali Wateja: Uzingatiaji wa mahitaji ya wateja na kutoa huduma bora.