Skip to main content

Miundombinu yetu

MUCE imesheheni miti ya asili na ya kupandwa, nyasi na maua. Kampasi hii ina eneo la Ekari 633.31, ambapo eneo lililoendelezwa ni Ekari 114.71, sawa na 18.11%, na eneo ambalo bado halijaendelezwa ni Ekari 518.60, sawa na 81.89% ya eneo lote. Matumizi ya ardhi iliyopo yamegawanywa katika maeneo mbalimbali. Ambayo ni eleo la utawala, eneo la mabweni ya wanafunzi, eneo la kituo cha afya, eneo la burudani, eneo la biashara na eneo la miliki. Eneo la Taalama ni 5.01% ya ardhi yote. Eneo hili linajumuisha Kumbi za Mihadhara, Vyumba vya Mihadhara, Vyumba vya Semina, Maabara za Sayansi, Maabara za Kompyuta, Kituo cha Rasilimali za Midia za Elimu na Maktaba.

Kumbi za Mihadhara

MUCE ina kumbi kubwa mbili za mihadhara zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,642: wanafunzi 1007 kwenye ukumbi wa kwanza wa mihadhara na 635 kwenye ukumbi wa pili.

Kumbi za Mihadhara

MUCE ina kumbi mbili za mihadhara zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 450: wanafunzi 250 kwenye ukumbumbi wa kwanza wa mihadhara na 200 kwenye ukumbi wa pili.

Vyumba vya Mihadhara na Semina

MUCE ina vyumba sita vya mihadhara vyenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 864. Pia, kuna vyumba saba vya semina vyenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 880.

Maabara za Sayansi

Kuna maabara saba zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 520 kwa wakati mmoja.

Maabara za Kompyuta

Kuna Maabara nne za Kompyuta zenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 216 kwa wakati mmoja.

Maktaba

MUCE ina Maktaba moja yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 523 kwa wakati mmoja.

Mabweni ya Wanafunzi

MUCE ina jumla ya mabweni sita yaliyopo ndani ya kampasi yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1,200.

KITUO CHA AFYA MKWAWA

Kituo cha Afya Mkwawa kinahudumia takribani watu elfu Hamsini (50,000) ambao wanajumuisha wanafunzi, wafanyakazi na jamii inayozunguka chuo. Kitengo cha Wagonjwa Wanaolazwa katika Kituo cha Afya kinajumuisha wodi za wanaume, wanawake na wodi la wagonjwa wanaolipia pesa tasilimu, lenye jumla ya vitanda arobaini na mbili (42). Kadhalika, kituo hiki kinafanya kazi saa ishirini na nne (24). Kinatoa ushauri wa kitabibu, uzazi wa mpango, vipimo vya maabara (damu, haja ndogo na haja kubwa), kusafisha na kufunga vidonda na kutoa dawa pamoja na vitengo mbalimbali vinavyosimamiwa na wafanyakazi wenye sifa ikiwa ni pamoja na Kitengo cha Wagonjwa wa Nje na Dharura, Kitengo cha Wagonjwa Wanaolazwa, Kliniki ya Uzazi na Afya ya Mtoto (RCH), Kitengo cha Matibabu ya Kuhara (DTC), Famasi, Maabara, Kitengo cha Ushauri Nasaha (VTC), Kliniki ya Dawa za Kufubaza Makali ya VVU (CTC), Kliniki ya Kifua Kikuu, Kitengo cha Afya ya Uzazi, Chumba cha Upasuaji Mdogo, na Mawodi ya Wanaume, Wanawake na Watu Binafsi.