**COMPUTER SHORT COURSES AT MUCE**
Mkwawa University College of Education (MUCE) kupitia Kitengo cha TEHAMA inatoa kozi fupi za kompyuta zenye lengo la kuwajengea washiriki ujuzi wa kisasa wa kidijitali unaohitajika katika masomo, kazi, na maisha ya kila siku. Kozi hizi zimeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya makundi mbalimbali ya watumiaji, kuanzia wanaoanza kabisa hadi wale wanaohitaji ujuzi wa hali ya juu.
