HEET Project Stakeholders Training on Gender Based Violence (GBV)
Tarehe 13 Septemba 2025, Chuo kimeendesha Mafunzo ya Ushirikishwaji wa Wadau juu ya masuala ya Ukatili wa Kijinsia (GBV) kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
🤝 Wadau mbalimbali wamekutana kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kuhusu mada hususani utekelezaji wa Mfumo wa KASEMA (One Stop Centre) unaotumiwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kukusanya maoni au malalamiko kuhusu utekelezaji wa Mradi.
Kabla ya mafunzo hayo, washiriki walipewa taarifa ya jumla kuhusu Mradi wa HEET hususani malengo ya mradi hasa kwa upande wa MUCE.
Mafunzo hayo yalifunguliwa na Naibu Rasi – Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Jaquiline Amani Moshi ambaye pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa mafunzo hayo ni muhimu na ni sehemu kubwa ya wajibu wa Chuo kuhakikisha wadau wote muhimu wanafahamu masuala yanayoendelea kwenye utekelezaji wa Mradi.
🗣️ Chuo kinatoa shukrani kwa washiriki wote waliofika kuhudhuria mafunzo hayo na kuwaomba wawe mabalozi kuhakikisha jumuiya nzima ya Chuo na nje ya Chuo wanapata elimu kuhusu Mradi ili kuepusha malalamiko yoyote.